Oman → Tanzania
Rate nzuri, risiti papo hapo, na unafuatilia kila order mpaka ifike Tanzania. Kwa simu, benki, LUKU na bili.
Huduma ya FastConnect Agency Limited · Kiasi cha chini OMR 1
1 OMR =
Rate ya leo haikupatikana kwa sasa. Uliza kwa WhatsApp — unajibiwa papo hapo.
Jinsi inavyofanya kazi
Hakuna fomu ndefu. Unatuma maelezo kwa ujumbe mmoja, unalipa OMR hapa Oman, na mpokeaji anapata TZS kwenye simu au akaunti yake.
Kwa WhatsApp au kwenye app: namba ya simu au akaunti, jina la mpokeaji, na kiasi (OMR). Mfano: 0712 345 678 Amina Juma 20.
Tunakuonyesha rate, TZS atakazopata na maelezo ya kulipia. Unalipa kwa benki au simu hapa Oman na kutuma picha ya risiti.
Wakala wetu Tanzania analipa, na unapata risiti ya malipo kwenye WhatsApp au app yako. Kwa LUKU, token inaonekana papo hapo.
Unatuma wapi?
Inaingia moja kwa moja kwenye laini ya mpokeaji.
Kwa akaunti za benki zote kuu za Tanzania na Zanzibar.
Lipa moja kwa moja kutoka Oman, na token au uthibitisho unakuja kwako.
Kwa nini WakalaOnline
Risiti ya wakala inakuja kama picha kwenye WhatsApp au app. Unaweza kuipakua kama PDF.
Inasubiri, inatumwa, imefika. Unaona hali ya order yako wakati wowote, bila kuuliza.
Ukituma kiasi kikubwa unapata rate maalum. Wateja wa kudumu wana rate yao.
Kila mteja ana code yake. Rafiki akitumia code yako, nyote mnapata bonus ya TZS.
Hesabu
Weka OMR unazotuma. Hesabu inatumia rate ya sasa; rate ya kiasi kikubwa inatumika yenyewe ukifika kiwango chake.
App ya WakalaOnline (Android)
Inafanya kazi moja kwa moja kwenye browser ya simu yoyote (Android na iPhone), bila kupakua. Unaingia kwa code ya WhatsApp; hakuna password ya kukumbuka.
Ukitaka iwe kama app ya kawaida: fungua wakalaonline.app/app kwenye Chrome au Safari, kisha chagua "Add to Home screen". Toleo la APK ni la Android na lina taarifa za simu (notifications).
Mawasiliano
Tuma ujumbe mmoja wenye namba, jina na kiasi. Ukijibiwa na bot, andika "ndiyo" kuthibitisha; mhudumu yupo kwa maswali mengine.
Fungua WhatsAppMara nyingi dakika chache baada ya malipo yako kuthibitishwa. Order za benki zinaweza kuchukua muda kidogo zaidi kulingana na benki.
Kwa benki au pesa ya simu hapa Oman. Maelezo ya akaunti unapewa baada ya kuthibitisha order, kisha unatuma picha ya risiti.
Wasiliana nasi mara moja kwa WhatsApp ukiwa na Ref ya order. Kabla malipo hayajathibitishwa, unaweza kughairi order kwenye app.
Rate inasasishwa kulingana na soko. Rate unayoiona wakati unathibitisha order ndiyo inayotumika.